• HABARI MPYA

  Wednesday, April 03, 2024

  SIMBA SC WAPO ANGANI WANAIFUATA AL AHLY KWA SHUGHULI YA IJUMAA


  BEKI Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’ akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam wakati wa safari ya kwenda Cairo, Misri Alfajiri ya leo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, Al Ahly Ijumaa.
  Simba watakuwa wageni wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa kuanzia Saa 5:00 usiku Uwanja wa Cairo international wakikabiliwa na shinikizo la kushinda ugenini kufuatia kufungwa 1-0 na mabingwa hao watetezi kwenye mechi ya kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla katí ya Al Ahly na Simba atakwenda kumenyana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.
  GONGA KUTAZAMA VÍDEO SIMBA WAKIWA SAFARINI 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPO ANGANI WANAIFUATA AL AHLY KWA SHUGHULI YA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top