• HABARI MPYA

  Wednesday, April 24, 2024

  YANGA SC YATOKA PATUPU ISAMUHYO, 0-0 NA JKT TANZANIA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Kwa sare hiyo, Yanga SC inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATOKA PATUPU ISAMUHYO, 0-0 NA JKT TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top