• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  CHAMA AINUSURU SIMBA KUPIGWA NA IHEFU SINGIDA, DROO 1-1


  VIGOGO, Simba SC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ihefu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. 
  Ihefu SC ambayo sasa inajulikana na Singida Black Stars ikiwa imehamishia maskani yake Singida chini ya umiliki mpya, kutoka Mbarali mkoani Mbeya ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na kiungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 41.
  Kiungo Mzambia, Clatous Chama akaisawazishia Simba SC kwa penalti dakika ya 72 kufuatia mshambuliaji Kibu Dennis Prosper kuchezewa rafu na beki wa Ihefu SC Mukrim Abdallah.
  Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Azam FC iliyocheza mechi moja zaidi na wote wapo nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 20.
  Kwa upande wao Ihefu SC sare hiyo inawafanya wafikishe pointi 24 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi ya tisa wakizidiwa wastani wa mabao tu na Kagera Sugar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA AINUSURU SIMBA KUPIGWA NA IHEFU SINGIDA, DROO 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top