• HABARI MPYA

  Sunday, April 28, 2024

  MAN CITY YAIBAMIZA NOTTINGHAM FOREST 2-0 THE CITY GROUND


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na beki wa miaka 22, Mcroatia Josko Gvardiol dakika ya 32 na mshambuliaji Mnorway Erling Braut Haaland (23) dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 79 katika mchezo wa 34 na inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na vinara, Arsenal waliocheza mechi 35, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 26 za mechi 35 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIBAMIZA NOTTINGHAM FOREST 2-0 THE CITY GROUND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top