• HABARI MPYA

  Monday, April 22, 2024

  BODI YAAHIRISHA MECHI ZA SIMBA NA AZAM, YAZIADHIBU TABORA, JKT NA KMC


  BODI ya Ligi Kuu (TPLB) imeahirisha mechi kadhaa za Azam na Simba ili kuzipa fursa ya kushiriki michuano ya Kombe la Muungano inayotarajiwa kuanza keshokutwa visiwani Zanzíbar.
  Simba itamenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu Fainali ya Kombe la Muungano Jumatano ya Aprili 24 Uwanja wa New Amaan Complex visiwani, Zanzíbar wakati Azam FC itaanza na KMKM Alhamisi.
  Washindi wa mechi za Nusu Fainali watakutana katika Fainali Aprili 27 hapo hapo Amaan Complex.
  Katika hatua nyingine, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imezitoza faini klabu za Tabora United, JKT Tanzania na KMC kwa makosa tofauti ya kikanuni kwenye mechi zao za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  GONGA KUSOMA ZAIDI ADHABU ZILIZOTOLEWA NA TPLB
  GONGA KUTAZAMA MECHI ZA LIGI KUU ZILIZOAHIRISHWA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BODI YAAHIRISHA MECHI ZA SIMBA NA AZAM, YAZIADHIBU TABORA, JKT NA KMC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top