• HABARI MPYA

  Friday, April 19, 2024

  LIVERPOOL YASHINDA LAKINI YAAGA UEFA EUROPA LEAGUE


  BAO la penalti la Mohamed Salah dakika ya saba limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Atalanta usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Gewiss mjini Berga katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali UEFA Europa League.
  Hata hivyo, ushindi huo haujatosha kuwapa Liverpool nafasi ya kuendelea na michuano kufuatia kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 11 Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool, hivyo wanatolewa kwa jumla ya mabao 3-1.
  Mechi nyingine za marudiano Robó Fainali UEFA Europa League usiku wa Alhamisi; AS Roma imeichapa AC Milan 2-1 na inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza.
  Nayo Bayer Leverkusen imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, West Ham United 1-1 na hivyo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mechi ya kwanza nyumbani.
  Nao Marseille wameitoa Benfica kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya jumla ya 2-2, wakifungwa 2-1 Ureno kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita kabla ya kushinda 1-0 jana Ufaransa.
  Katika Nusu Fainali za UEFA Europa League, Marseille itamenyana na Atalanta na Roma dhidi ya Bayer Leverkusen na mechi za kwanza zitafanyika Mei 2 na marudiano Mei 9. 
  Marseille na Roma wataanzia nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YASHINDA LAKINI YAAGA UEFA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top