• HABARI MPYA

  Sunday, April 14, 2024

  AZAM FC YAWACHAPA NAMUNGO FC 2-0 PALE PALE RUANGWA


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Shujaa wa Azam FC katika mchezo wa leo ni winga Muivory Coast, Kipre Tiagori Emmanuel Junior Zunon aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 62 na 84.
  Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 50 katika mechi ya 22, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mchezo mmoja mkononi.
  Kwa upande wao Namungo FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 23 za mechi 22 nafasi ya 11.
  iframe width="1236" height="695" src="https://www.youtube.com/embed/p1MPsFePLZg" title="Magoli | Namungo FC 0-2 Azam FC | NBC Premier League | NBC Premier League 14/04/2024" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture; web-share" referrerpolicy="strict-origin-when-cross-origin" allowfullscreen>
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWACHAPA NAMUNGO FC 2-0 PALE PALE RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top