• HABARI MPYA

  Friday, April 12, 2024

  ATALANTA YAITANDIKA LIVERPOOL 3-0 PALE PALE ANFIELD EUROPA LEAGUE


  WENYEJI, Liverpool wametandikwa mabao 3-0 na Atalanta ya Italia katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali michuano ya UEFA Europa League usiku wa Alhamisi Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool, England.
  Kiboko ya Liverpool usiku huu ni mshambuliaji wa zamani wa West Ham ya United ya England pia, Gianluca Scamacca aliyefunga mabao mawili dakika ya 35 na 60, huku bao la tatu la Atalanta likifungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Croatia mzaliwa wa Ujerumani, Mario Pasalic dakika ya 83.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 18 Uwanja wa Gewiss mjini Bergamo nchini Italia na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Benfica ya Ureno na Marseille ya Ufaransa.
  Mechi nyingine za kwanza za Robo Fainali UEFA Europa League, AS Roma imewachapa AC Milan 1-0,  Bayer Leverkusen imewachapa West Ham 2-0 na Benfica imewachapa Marseille 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ATALANTA YAITANDIKA LIVERPOOL 3-0 PALE PALE ANFIELD EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top