• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2024

  WAZIRI WA MICHEZO DK NDUMBARO AKIONYESHA UMAHIRI WAKE KWENYE GOFU


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro Aprili 14, 2024 amekuwa Mgeni Rasmi wakati wa Fainali za mashindano maalumu ya gofu ya Lina PG Tour yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkana mjini Morogoro.
  Mashindano hayo yameandaliwa na Familia ya Lina Nkya aliyekuwa mchezaji mkongwe wa gofu nchini na mmoja wa viongozi wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) wakati wa uhai wake kwa lengo la kutambua mchango wake kwenye maendeleo ya mchezo huo ambapo pia vilabu kutoka mikoa mbalimbali vimeshiriki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO DK NDUMBARO AKIONYESHA UMAHIRI WAKE KWENYE GOFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top