• HABARI MPYA

  Thursday, April 25, 2024

  MAN UNITED YAICHIMBIA KABURI SHEFFIELD UNITED, YAICHAPA 4-2


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na beki Muingereza, Jacob Harry Maguire dakika ya 42, kiungo Mreno, Bruno Fernandes mawili, la penalti dakika ya 61 na dakika ya 81 na la nne mshambuliaji Mdenmark, Rasmus Højlund dakika ya 85, wakati ya Sheffield United yamefungwa na beki Muingereza, Jayden Bogle dakika ya 35 na mshambuliaji Mchile, Benjamin
  Brereton dakika ya 50.
  Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 53 katika mchezo wa 33 na kusogea nafasi ya sita wakiizidi pointi tatu Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 33.
  Kwa upande wao Sheffield United hali inazidi kuwa mbaya baada ya kupoteza mchezo huo, kwani wanabaki mkiani na pointi zao 16 za mechi 34.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHIMBIA KABURI SHEFFIELD UNITED, YAICHAPA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top