• HABARI MPYA

    Monday, April 08, 2024

    BEKI WA ZAMANI WA YANGA SULEIMAN MKATI AFARIKI DUNIA TEMEKE

    Suleiman Mkati (wa kwanza kulia) akiwa na wachezaji wenzake wa Yanga mwaka 1991, Abdallah Suleman Kaburu na Kenneth Pius Mkapa kabla ya moja ya mechi zao  

    ALIYEWAHI kuwa beki wa kulia wa klabu ya Yanga, Suleiman Abdallah Mkati amefariki dunia leo katika hospitali ya Temeke alipopelekwa kwa matibabu akiwa ana umri wa miaka 53.
    Suleiman Abdallah Mkati aliyezaliwa Desemba 18, 1969, aliibukia katika klabu ya Sigara FC ambako alicheza kuanzia mwaka 1984 hadi 1989 akahamia Pilsner, zote za Dar es Salaam.
    Suleiman Mkati, kulia waliosimama akiwa na kikosi cha Yanga cha mwaka 1994 ambao ndio ulikuwa msimu wake wa mwisho Jangwani.
    Suleiman Mkati, wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na kikosi cha Yanga cha mwaka 1994 ambao ndio ulikuwa msimu wake wa mwisho Jangwani.

    Alicheza Pislner hadi mwaka 1991 aliposajiliwa na vigogo wa soka nchini, Yanga SC ambako alidumu hadi mwaka 1995 aliporejea Sigara ambako alicheza tena hadi mwaka 1997.
    Mwaka 1998 akachukuliwa na wa jina lake, Suleiman Mathew kwenda kuisaidia timu ya Mto ya Singida, baadaye Singida United 2000 kupanda Ligi Kuu na ilipopanda tu mwaka 1999 Mkati akastaafu soka.
    Mkati ambaye pia alicheza timu ya taifa kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1991 - baada ya kustaafu soka alipata mafunzo mbalimbali ya ukocha.
    Msiba upo nyumbani kwao, Tandika Maghorofani na mwili wake utasafirishwa kesho Saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Visiga, Kibaha mkoani Pwani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI WA ZAMANI WA YANGA SULEIMAN MKATI AFARIKI DUNIA TEMEKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top