• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2024

  BAYERN MUNICH YAIGOMEA ARSENAL LONDON, 2-2

  WENYEJI, Arsenal FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Emirates Jijini London, Englands.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na washambuliaji, ‘bwana mdogo’ wa miaka 22 Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Bukayo Saka dakika ya 12 na Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 76.
  Kwa upande wao Bayern Munich ilipata mabao yake kupitia kwa washambuliaji wake, Mjerumani Serge Gnabry dakika ya na 18 na Muingereza Harry Kane kwa penalti dakika ya 32.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 17 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Real Madrid ya Hispania na Manchester City ya England pia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH YAIGOMEA ARSENAL LONDON, 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top