TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Msenegal, Libasse Guèye dakika ya 20, mabeki Nickson Clement Kibabage dakika ya 55, Rushine De Reuck raia wa Afrika Kusini dakika ya 75 kwa penalti na kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama dakika ya 79.
Simba SC sasa inasubiri mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kati ya Azam FC na mabingwa watetezi, Yanga SC wakutane naye kwenye Fainali baadaye mwezi huu.



.png)
0 comments:
Post a Comment