• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2024

  MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA YANGA KARUME SONGORO AFARIKI DUNIA

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Karume Songoro (43) amefariki dunia leo huko Kahama alipokuwa anaishi na familia yake baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Saratani ya Misuli kwa muda mrefu.
  Karume Songoro aliyezaliwa Machi 24, 1982 aliibukia Buluba ya Shinyanga, kabla ya kuhamia Lumumba Rovers na baadaye Toto African zote za Mwanza mwaka 1998.
  Mwaka 1999 alisajiliwa Yanga SC ambako baada ya miezi kadhaa akaachwa na kutimkia 82 Rangers ya Shinyanga ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa Kahama United kufuatia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kujivua umiliki.
  Mwaka 2004 akaenda Moro United hadi mwaka 2005 akahamia Kagera Sugar, kabla ya kwenda Rwanda kuchezea Rayon Sport.
  Mara ya mwisho Karume Songoro ambaye amewahi pia kuchezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars - alichezea timu ya Geita Gold Mine nam mwaka 2014-215.

  Karume Songoro alipokuwa anacheza Yanga SC mwaka 1999
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA YANGA KARUME SONGORO AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top