• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2024

  ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND


  TIMU ya Arsenal jana imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Mabao ya mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 45 na kiungo Mnorway, Martin Ødegaard dakika ya 90'+5 na kwa ushindi huo, Arsenal wanafikisha pointi 74 katika mchezo wa 33 na kurejea kileleni wakiwazidi pointi moja tu mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Wolverhampton Wanderers baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao43 za mechi 33 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top