• HABARI MPYA

  Monday, April 29, 2024

  ZAMALEK YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


  TIMU ya Zamalek SC ya Misri imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Dreams FC Uwanja wa Baba Yara Stadium Jijini Kumasi nchini Ghana.
  Mabao ya Zamalek yalifungwa na beki Mtunisia, Hamza Mathlouthi dakika ya 12, mshambuliaji Mbenin Samson Akinyoola dakika ya 27 na kiungo Mmisri,  Mostafa Shalaby dakika ya 59.
  Zamalek inakwenda Fainali kwa ushindi huo wa ugenini baada ya sare ya bila kufungana na Dreams kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Cairo nchini Misri na sasa itakutana na RSB Berkane ya Morocco iliyofuzu bila jasho kufuatia mabingwa watetezi, USM Alger kutotokea uwanjani jana Jijini Berkane.
  Ikumbukwe mechi ya kwanza pia haikuchezwa baada ya USM Alger kuwazuia RSB Berkane kucheza wakiwa na jezi zenye bendera ya Morocco kutokana na mzozo wa Kidiplomasia unaoendelea baina ya nchi hizo mbili.
  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likaiadhibu USM Alger kwa kuipa RSB Berkane ushindi wa mabao 3-0 na kuitaka kwenda Morocco kwa mchezo wa marudiano.
  Katika Fainali Kombe la Shirikisho, RSB Berkane wataanzia nyumbani Jumapili ya Mei 12 Uwanja wa Manispaa ya Berkane, wakati Zamalek watamalizia nyumbani Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo Jumapili ya Mei 19.
  Ikumbukwe na Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika pia Esperance itaanzia nyumbani Jumamosi ya Mei 18 Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi Jijini Radès nchini Tunisia, kabla ya timu hizo kurudiana Mei Jumamosi ya Mei 25 Uwanja wa CairoInternational Jijini Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMALEK YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top