• HABARI MPYA

    Friday, April 19, 2024

    AZAM FC YASAJILI BEKI WA MALI YORO MAMADOU DIABY


    KLABU ya Azam FC imefikia makubaliano na akademi ya Yeleen Olympique ya Mali kwa ajili ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Yoro Mamadou Diaby.
    Taarifa ya Azam FC imesema kwamba beki huyo wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Stade Malien de Bamako, atajiunga nao rasmi kuanzia msimu ujao wa 2024/25.
    Akiwa klabuni Stade Malien de Bamako, Yoro aliisadia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho, akiifungia timu yake mabao katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Dreams FC ya Ghana.
    Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23.
    Yoro pia alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI BEKI WA MALI YORO MAMADOU DIABY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top