• HABARI MPYA

  Friday, April 12, 2024

  COASTAL UNION YAICHAPA MASHUJAA 2-1 PALE PALE KIGOMA


  TIMU ya Coastal Unión imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Mabao ya Coastal Unión yamefungwa na Shedrack Malungwe dakika ya 10 na Bakari Suleiman dakika ya 57, wakati bao pekee la Mashujaa FC limefungwa na Omar Omar dakika ya 45.
  Kwa ushindi huo, Coastal Unión inafikisha pointi 33, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake 21 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA MASHUJAA 2-1 PALE PALE KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top