• HABARI MPYA

  Monday, April 08, 2024

  YANGA WAWASILI DODOMA KUTETEA KOMBE LA TFF JUMATANO


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamewasili jioni ya leo Jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC keshokutwa kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Ikumbukwe Simba SC wamewasili Kigoma mapema leo tayari kwa mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la TFF dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC kesho kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Lake Tanganyika.
  Tayari timu sita zimekwishatinga Robo Fainali ambazo ni Azam FC, Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.
  GONGA KUTAZAMA VIDEO ILIVYOWASILI DODOMA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAWASILI DODOMA KUTETEA KOMBE LA TFF JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top