• HABARI MPYA

  Sunday, April 14, 2024

  ASTON VILLA YAWACHAPA ARSENAL 2-0 PALE PALE EMIRATES


  MATUMAINI ya Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England yameanza kupangua baada ya leo kuchapwa mabao 2-0 nyumbani na Aston Villa Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao yaliyozamisha Arsenal leo yamefungwa na kiungo Mjamaica, Leon Bailey dakika ya 84 na mshambuliaji Muingereza, Ollie Watkins dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo, Aston Villa inafikisha pointi 60 katika mchezo wa 33 na kupanda nafasi ya nne, ikiizidi tu wastani wa mabao Tottenham Hotspur ambayo imecheza mechi 32.
  Kwa upande wao Arsenal baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 71 nafasi ya pili wakiizidi wastani wa mabao Liverpool na wote wakiwa nyuma ya Manchester City wenye pointi 73 baada ya timu zote kucheza mechi 32.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ASTON VILLA YAWACHAPA ARSENAL 2-0 PALE PALE EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top