• HABARI MPYA

  Wednesday, April 17, 2024

  KAGERA SUGAR YAIKANDA TABORA UNITED 3-0 PALE PALE MWINYI


  TIMU ya Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na kiungo Moubarak Hamza dakika ya 24 na washambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 48 na mzawa Mbaraka Yussuf dakika ya 72.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya saba, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 22 za mechi 23 sasa nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAIKANDA TABORA UNITED 3-0 PALE PALE MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top