• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2024

  RAIS YANGA AMKABIDHI WAZIRI MKUU MSTAAFU DK. MALECELA ‘UZI’ WA WANANCHI


  RAIS wa Yanga SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Klabu Afrika, Hersi Ally Said leo amepata mwaliko wa kumtembelea na kumjulia hali Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Samuel Malecela nyumbani kwake Jijini Dodoma. 
  Yanga ipo Dodoma kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC leo kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Jamhuri.
  Tayari timu saba zimetinga Robo Fainali ya michuano hiyo ambazo ni Mashujaa FC, Azam FC, Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS YANGA AMKABIDHI WAZIRI MKUU MSTAAFU DK. MALECELA ‘UZI’ WA WANANCHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top