• HABARI MPYA

  Wednesday, April 24, 2024

  KAI APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA CHELSEA 5-0


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi mnono dhidi ya Chelsea wa mabao 5-0 usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na mshambuliaji, Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya nne, beki Muingereza Benjamin White dakika ya 52 na 70 na kiungo Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 57 na 65.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 77 katika mchezo wa 34 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool iliyocheza mechi 33 na wote wakiwa mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 73 za mechi 32.
  Kwa upande wao Chelsea waliokuwa wanacheza mechi ya 32 ya msimu wanabaki na pointi zao 47 katika nafasi ya tisa baada ya kupoteza mchezo wa leo dhidi ya mahasimu wao wa London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAI APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA CHELSEA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top