• HABARI MPYA

    Friday, April 12, 2024

    PRISONS NA KMC HAKUNA MBABE, 1-1 SOKOINE


    WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Abdulkarim Abdullah alianza kuifungia KMC dakika ya 10, kabla ya Ibrahim Abraham kuisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 81.
    Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi 29, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakiendelea kuizidi wastani wa mabao KMC baada ya wote kucheza mechi 22.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PRISONS NA KMC HAKUNA MBABE, 1-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top