• HABARI MPYA

  Thursday, April 18, 2024

  BAYERN MUNICH YAICHAPA ARSENAL 1-0 KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, Bayern Munich wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal ya England usiku huu Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani, Joshua Walter Kimmich dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri ya beki Mreno, mzaliwa wa Ufaransa,  Raphaël Guerreiro.
  Bayern Munich wanatinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 9 Uwanja Emirates Jijini London.
  Sasa Bayern Munich watakutana na mshindi kati ya Real Madrid na mabingwa watetezi, Manchester City katika Nusu Fainali Aprili 30 Ujerumani na marudiano Mei 7 ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH YAICHAPA ARSENAL 1-0 KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top