• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  KEN GOLD NA PAMBA ZABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA USHINDI LEO


  WENYEJI, Pamba FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Talents katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mechi nyingine za NBC Championship leo Copco United imechapwa 1-0 na Polisi Tanzania Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mbeya Kwanza imeichapa Pan Africans 2-0 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mbeya City imeichapa Mbuni FC 2-1 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Ken Gold imeichapa TMA 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha, Biashara United imeitandika Green Warriors 3-0 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Transit Camp imeichapa Stand United 3-0 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Cosmo Politana imeilaza Ruvu Shooting 1-0 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkaoni Pwani.  
  Kuelekea mechi mbili za mwisho msimamo wa NBC Championship sasa ni; Ken Gold pointi 64, Pamba FC 61, Biashara United na Mbeya Kwanza 59 kila moja, TMA 54, Mbuni na Mbeya City 42 kila moja, Polisi Tanzania 38, Cosmopolitan 36, Fountain Gate Talent na Stand United 31 kila moja, Green Warriors 28, Transit Camp 26, Copco 19, Pan Africans 16 na Ruvu Shooting 12 baada ya timu zote kucheza mechi 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KEN GOLD NA PAMBA ZABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA USHINDI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top