• HABARI MPYA

  Monday, April 08, 2024

  AZAM FC YATOA SEMINA YA UKUZAJI VIPAJI KWA VITUO 10


  KLABU ya Azam FC imeendesha semina maalumu ya kutoa miongozo kwa vituo 10 vya kukuza vipaji, tulivyoingia navyo mikataba ya ushirikiano.
  Miongozo hiyo ilikuwa ikitolewa na wataalamu wetu wa benchi la ufundi la Azam FC Academy, akiwemo Mtaalamu wa Sayansi ya Michezo, Nyasha Charandura.
  Baadhi ya miongozo hiyo ni vituo hivyo kupewa aina ya vipaji vinavyotakiwa kuvunwa, njia sahihi za kuwandaa wachezaji hao kulingana na utamaduni na falsafa ya klabu yetu.
  Mara baada ya kuifunga semina hiyo elekezi ya siku tatu, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Omary Kuwe, aliwaasa makocha wa vituo hivyo kuzingatia miongozo yote waliyopewa, ili kufanikisha mafanikio yaliyokusudiwa kwenye mradi huo.
  Katika hatua nyingine, Kuwe alitoa seti za jezi, mipira na vifaa vya mazoezi kwa vituo vyote hivyo, vitakavyowasaidia katika kazi yao.
  Azam FC inaamini kuwa ndani ya miaka michache ijayo itaweza kujipatia vipaji bora kupitia mradi wetu huu wa ushirikiano na vituo hivyo, yaani Azam FC Centers.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATOA SEMINA YA UKUZAJI VIPAJI KWA VITUO 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top