• HABARI MPYA

  Monday, April 29, 2024

  JKT TANZANIA YAICHIMBIA KABURI MTIBWA SUGAR, YAICHAPA 2-1 MBWENI


  WENYEJI, JKT Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Edson Katanga dakika ya saba na Sixtus Sabilo dakika ya 90, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Charles Ilamfya dakika ya 22.
  Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 24 na kusogea nafasi ya 10, wakati Mtibwa Sugar inabaki nafasi ya mwisho kwenye Ligi ya timu 16 ikiwa na pointi 17 za mechi 23 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHIMBIA KABURI MTIBWA SUGAR, YAICHAPA 2-1 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top