• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  JKT TANZANIA YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO 1-1 NA TABORA UNITED


  WENYEJI, Tabora United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Tabora United ilitangulia kwa bao la beki Mkongo, Heritier Lulihoshi dakika ya 72 kwa penalti, kabla ya kiungo Martin Kiggi kuisawazishia JKT Tanzania dakika ya 90+2.
  Kwa matokeo hayo, Tabora United inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi ya 12, wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 21 za mechi 21 katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka na mbili zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini kuwania kubaki Ligi Kuu, wakati itakayofungwa itakwenda kujaribu tena kujinusuru kwa kucheza na timu ya Championship.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO 1-1 NA TABORA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top