• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE KWA DODOMA JIJI, 1-1 KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Dodoma Jiji FC walitangulia kwa bao la winga Iddi Bahati Kipagwile dakika ya 11, kabla ya mshambuliaji Moubarak Hamza kuisawazishia Kagera Sugar kwa penalti dakika ya 48.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 22 nafasi ya saba, wakati Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 21 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE KWA DODOMA JIJI, 1-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top