• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2024

  FEISAL AWAZIMA IHEFU CHAMAZI, AZAM YASHINDA 1-0


  BAO pekee la kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 13 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao Ihefu SC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 25 za mechi 24 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEISAL AWAZIMA IHEFU CHAMAZI, AZAM YASHINDA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top