• HABARI MPYA

  Tuesday, April 16, 2024

  DODOMA JIJI YATOA SULUHU NA JKT TANZANIA LEO JAMHURI


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya mabao na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Matokeo hayo yanaifanya Dodoma Jiji FC ifikishe pointi 25 katika nafasi ya saba na JKT Tanzania imefikisha pointi 22 nafasi ya 12 katika Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 22.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YATOA SULUHU NA JKT TANZANIA LEO JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top