• HABARI MPYA

  Saturday, April 13, 2024

  MAN CITY YAIKANDAMIZIA 5-1 LUTON TOWN NA KUREJEA KILELENI ENGLAND


  MABINGWA watetezi, Manchester City leo wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Luton Town Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Beki Mjapan, Daiki Hashioka alijifunga dakika ya pili baada ya kugongwa na mpira uliopigwa kwa tik-tak na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland ambaye pia alifunga bao la tatu dakika ya 76 kwa penalti.
  Mabao mengine ya Man City yamefungwa na kiungo Mcroatia, Mateo Kovačić dakika ya 64 na mshambuliaji Mbelgiji mwenye asili ya Ghana, Jérémy Doku dakika ya 87 na beki Mcroatia, Joško Gvardiol dakika ya  90'+3, wakati bao pekee la Luton Town limefungwa na beki Muingereza, Ross Barkley dakika ya 81.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 73 katika mchezo wa 32 na kurejea kileleni, wakizizidi pointi mbili kila moja, Arsenal na Liverpool ambazo zimecheza mechi 31 - wakati Luton Town wanabaki na pointi 25 za mechi 33 sasa nafasi ya 18. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIKANDAMIZIA 5-1 LUTON TOWN NA KUREJEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top