• HABARI MPYA

  Thursday, April 25, 2024

  AZAM YAICHAPA KMKM 5-2 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA MUUNGANO


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya KMKM katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili, dakika ya saba na 42, Nathaniel Chilambo dakika ya tisa, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 49 na Iddi Kichindo dakika ya 74, wakati ya KMKM yamefungwa na Abrahman Ali yote kwa penalti dakika ya 38 na.
  Azam FC sasa itakutana na Simba SC katika Fainali hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex kuhitimisha sherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzíbar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Simba SC ilikata tiketi ya Fainali jana kwa ushindi wa mabao 2-0, mabao ya Muivory Coast Freddy Michael Koublan na mzawa, Israel Patrick Mwenda dhidi ya wenyeji wengine, KVZ hapo hapo New Amaan Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAICHAPA KMKM 5-2 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA MUUNGANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top