• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2024

  SERIKALI YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA FIFA KUINUA SOKA NCHINI


  KATIBU Mkuu wa Wizara Utamaduni Sanaa, Gerson Msigwa, Gerson Msigwa amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), wataunga mkono juhudi zinazoletwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA) katika kuleta maendeleo ya soka la vijana kuanzia ngazi ya chini.
  Kauli hiyo ameitoa leo Machi 15, 2024 wakati akizindua mafunzo ya mpira wa miguu kwa ajili ya kufundisha watoto kwenye shule iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA na Shirikisho la mpira Barani Afrika (CAF) kwa ajili ya mafunzo kwa walimu 46 kutoka shuleni za msingi kutoka wilaya 16 nchini.
  Msigwa, amewataka walimu waliopata mafunzo hayo kuyazingatia na kwenda kuwapa ujuzi huo watoto katika shule.
  Alisema programu hiyo imekuja kimkakati kwa sababu nchi imeenda kuwekeza katika michezo kuanzia chini.
  "Niwapongeze TFF kwa kuwa na uhusiano mzuri na FIFA na CAF,"alisema na kuongeza;
  “Kwa sasa hatutalala na kukubali hizi juhudi zipotee, zinazotokana na mahusiano mazuri baina ya TFF na FIFA pamoja na CAF, walimu waliofaidika na programu hii wakahakikishe wanawatengeneza vijana vizuri," alisisitiza
  Program hii ya mpira shuleni ni kitu muhimu sana kwa sabahu kuna vipaji vingi lakini hawapati nafasi ila hii inaweza kusaidia kwa taifa letu kwa siku za mbele,” alisema Msigwa.
  Aliongeza kuwa nchi itakuwa mwenyeji wa AFCON 2027, kunatakiwa kuwa na maandalizi makubwa ikiwemo kuandaa timu za Taifa na inaanzia shuleni, walimu wanatakiwa kutumia vizuri mifumo hii maalum kuwapika vijana wa kesho.
  “Tulipotoka huko nyuma tulikuwa na vipaji lakini sasa wanatakiwa kutengenezwa na kujua waishi vipi kimichezo, na Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza katika michezo na inafanya kwa vitendo.
  Naye Rais wa TFF, Wallace Karia alisema programu hiyo muhimu ni kwa ajili ya watoto kuanzia miaka 6 hadi 14 na wameanza kwenye shule.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA FIFA KUINUA SOKA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top