• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2024

  GEITA GOLD YAAMBULIA SULUHU KWA TABORA UNITED


  TIMU ya Tabora United imelazimishwa sare ya bila kufungana na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Kwa matokeo hayo, Tabora United inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya 13, wakati Geita Gold imetimiza pointi 24, ingawa inabaki nafasi ya 12 katika Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 24.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAAMBULIA SULUHU KWA TABORA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top