• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2024

  MANCHESTER CITY YATOA SARE NA REAL 3-3 BERNABEU


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamelazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na wenyeji, Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Bernardo Silva dakika ya pili, Philip Foden dakika ya 66 na Joško Gvardiol dakika ya 71, wakati ya Real Madrid yamefungwa na Rúben Dias aliyejifunga dakika ya 12, Rodrygo dakika ya 14 na Federico Valverde dakika ya 79.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 17 Uwanja wa Etihad Jijini Manchester na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Arsenal na Bayern Munich katika Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YATOA SARE NA REAL 3-3 BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top