• HABARI MPYA

  Tuesday, April 30, 2024

  SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO FC 2-2 RUANGWA


  WENYEJI, Namungo FC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Simba walitangulia kwa bao la mshambuliaji Mcameroon, Leandre Willy Essomba Onana dakika ya 34, kabla ya mshambuliaji mzawa, Kelvin Sabato Kiduku kuisawazishia Namungo FC dakika ya 39.
  Kipindi cha pili tena Simba walitangulia kwa bao la kiungo Edwin Balua dakika ya 70, kabla ya beki Kennedy Wilson Juma kujifunga dakika ya 90 kuisawazishia Namungo FC.
  Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 24 nafasi ya tisa, wakati Simba SC inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 22 nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 na Yanga 62 baada ya wote kucheza mechi 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO FC 2-2 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top