• HABARI MPYA

  Tuesday, April 30, 2024

  AZAM FC YASAJILI KIFAA KINGINE CHA STADE MALIEN


  KLABU ya Azam FC imemsajili kiungo mshambuliaji wao, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien ya Mali kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao 2024/25.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa pili kusainishwa mkataba Azam FC hata kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, baada ya beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien pia ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali.
  “Tumefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) ya kumsajili kiungo mshambuliaji wao, Franck Tiesse,” imesema taarifa ya Azam FC.
  Tiesse anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, akiwa Stade Malien aliisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI KIFAA KINGINE CHA STADE MALIEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top