• HABARI MPYA

  Sunday, April 28, 2024

  ARSENAL YAICHAPA SPURS 3-2 UWANJA WA TOTTENHAM HOTSPUR


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na kiungo Mdenmark, Pierre-Emile Hojbjerg aliyejifunga dakika ya 15, mshambuliaji Muingereza Bukayo Saka dakika ya 27 na kiungo Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 38, wakati ya Tottenham Hotspur yamefungwa na beki Muargentina, Cristian Romero dakika ya na 64 na mshambuliaji Mkorea Kusini, Son Heung-Min kwa penalti dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 80 katika mchezo wa 35 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao wana pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Tottenham Hotspur wanabaki na pointi zao 60 za mechi 33 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA SPURS 3-2 UWANJA WA TOTTENHAM HOTSPUR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top