• HABARI MPYA

  Saturday, April 06, 2024

  ARSENAL YAICHAPA BRIGHTON 3-0 NA KUREJEA KILELENI MWA LIGI KUU ENGLAND


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa AMEX, Falmer, East Sussex.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na mshambuliaji Muingereza Bukayo Saka dakika ya 33 kwa penalti, kiungo mshambuliaji Kai Havertz dakika ya 62 na mshambuliaji Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 71 katika mchezo wa 31 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiizidi pointi moja Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati mabingwa watetezi, Manchester City wanarudi nafasi ya tatu kwa pointi zao 70 za mechi 31 pia.
  Kwa upande wao, Brighton & Hove Albion  baada ya kupoteza mchezo wa leo nyumbani wanabaki na pointi zao 43 za mechi 31 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA BRIGHTON 3-0 NA KUREJEA KILELENI MWA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top