• HABARI MPYA

  Saturday, April 27, 2024

  MAN UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 KWA BURNLEY


  WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Burnley FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester/
  Mshambuliaji Mbrazil, Antony Matheus dos Santos alianza kuifungia Manchester United dakika ya 79, kabla ya mshambuliaji Mswisi mwenye asili ya Tunisia, Mohamed Zeki Amdouni kuisawazishia Burnley kwa penalti dakika ya 87.
  Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 54 katika nafasi ya sita ikiizidi tu pointi moja Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Burnley inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 35 nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 KWA BURNLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top