• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2024

  YANGA SC WATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE LA CRDB FEDERATION


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Augustino Samson Nsata aliyejifunga akijaribu kuokoa krosi ya winga Mghana, Augustino Okrah dakika ya tatu na mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 66.
  Winga Iddi Bahati Kipawgwile aliikosesha Dodoma Jiji bao dakika ya 51 baada ya kupiga nje mkwaju wa penalti ulitolewa kufuatia Mudathir Yahya Abbas kumchezea rafu mshambuliaji Mghana, Christian Zigah.
  Yanga inaungana na Mashujaa FC, Azam FC, Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United kukamilisha timu nane za Robo Fainali.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE LA CRDB FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top