• HABARI MPYA

  Monday, April 15, 2024

  MO DEWJI AKUTANA NA VIONGOZI SIMBA KUWEKA MAMBO SAWA WAIFUNGE YANGA


  RAIS wa Heshima wa klabu ya Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji amesema kwamba amekutana na viongozi kwa mazungumzo juu ya changamoto zinazoikabili timu ya soka na kwamba kila kitu kimeenda vizuri.
  Mo Dewji amesema hayo kuelekea mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  “Nimefanya kikao na viongozi wa Simba SC kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua. Kikao kimeenda vizuri. WanaSimba tusife moyo, tuendele kushirikiana,”amesema Mo Dewji.
  Simba SC imetoka kucheza mechi nne bila ushindi, mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly wakifungwa 1-0 nyumbani na 2-0 ugenini, moja ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Mashujaa walifungwa kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 Kigoma na nyingine ya Ligi Kuu waliyotoa sare ya 1-1 na Ihefu juzi mjini Singida.
  Na baada ya matokeo hayo zikaibuka lawama dhidi ya Mo Dewji ambaye pia ni mwekezaji katika klabu hiyo kwamba hatoi Fedha ndiyo maana timu inayumba kwa sababu inaendeshwa kwa michango ya viongozi baina yao.
  Wazi kikao cha leo kinaweza kikawa suluhisho la matatizo ya klabu japo kwa muda mfupi. 
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MO DEWJI AKUTANA NA VIONGOZI SIMBA KUWEKA MAMBO SAWA WAIFUNGE YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top