• HABARI MPYA

  Monday, April 08, 2024

  SIMBA SC YAWASILI KIGOMA KUIVAA MASHUJAA KESHO KOMBE LA TFF


  KIKOSI cha Simba kimewasili salama Kigoma tayari kwa mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC kesho kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Lake Tanganyika.
  Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo itakamilishwa kesho kwa mchezo kati ya Mabingwa watetezi, Yanga SC dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Tayari timu sita zimekwishatinga Robo Fainali ambazo ni Azam FC, Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI SIMBA ILIVYOWASIKI KIGOMA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWASILI KIGOMA KUIVAA MASHUJAA KESHO KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top