• HABARI MPYA

  Wednesday, April 17, 2024

  GEITA GOLD YATOKA SULUHU NA TANZANIA PRISONS NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold leo wamelazimishwa sare ya bila mabao na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania leo Uwanja wa sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 23 nafasi ya 13, wakati Tanzania Prisons imefikisha pointi 30 katika mchezo wa 23 nafasi ya sita.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YATOKA SULUHU NA TANZANIA PRISONS NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top