• HABARI MPYA

  Wednesday, April 17, 2024

  YANGA NA TABORA UNITED, AZAM FC NA NAMUNGO ROBO FAINALI KOMBE LA TFF


  MABINGWA watetezi, Yanga SC watamenyana na Tabora United katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup 
  Katika droo iliyopangwa leo studio za AzamSports, washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC watamenyana na Namungo FC, Coastal Union na Geita Gold na Ihefu SC dhidi ya Mashujaa FC.
  Mechi hizo za Robo Fainali zitafanyika kuanzia Mei 2 hadi 3, wakati Nusu Fainali zitafuatia Mei 18 na 19.
  Katika Nusu Fainali, mshindi wa Robo Fainali kati ya Azam FC na Namungo atakutana na mshindi kati ya Coastal Union na Geita Gold, wakati mshindi kati ya Yanga  na Tabora United atakutana na mshindi kati ya Ihefu na Mashujaa FC, wakati Fainali itapigwa Juni 2 Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA TABORA UNITED, AZAM FC NA NAMUNGO ROBO FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top