• HABARI MPYA

  Saturday, April 27, 2024

  NI SIMBA SC MABINGWA WA KWANZA MUUNGANO CUP, WAICHAPA AZAM 1-0 ZANZÍBAR


  TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutwaa Kombe la Muungano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Fainali usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Msenegal, Babacar Sarr, dakika ya 77 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Israel Patrick Mwenda kufuatia mshambuliaji Mcameroon, Leandre Willy Essomba Onana kuangushwa nje kidogo ya boksi.
  Kwa ushindi huo, Simba SC imezawadiwa Sh. Milioni 50, wakati washindi wa pili, Azam FC wamepata Sh. Milioni 30.
  Hilo linakuwa taji la pili kwa Simba SC msimu huu baada ya kuanza na taji la Ngao ya Jamii wakimfunga mtani, Yanga Agosti mwaka jana Jijini Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SIMBA SC MABINGWA WA KWANZA MUUNGANO CUP, WAICHAPA AZAM 1-0 ZANZÍBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top