• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2024

  NI MAMELODI NA ESPERANCE NA AHLY NA MAZEMBE NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  TIMU za TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Esperance ya Tunisia zimefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuzitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Petró Atletico Luanda ya Angola.
  Mazembe jana ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Petró Atletico Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda, hivyo kusonga mbele kufuatia sare ya bila kwenye mchezo wa kwanza Lubumbashi wiki iliyopita.
  Katika mchezo wa jana, Petró Atletico walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Honduras, Jonathan Toro dakika ya 29, kabla ya Mazembe kutoka nyuma kwa mabao ya washambuliaji Philippe Kinzumbi dakika ya 82 na Joël Beya dakika ya 90.
  Mazembe sasa itakutana na Al Ahly ambayo iliitoa Simba na Tanzania kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani.
  Kwa upande wao Espérance jana walilazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, ASEC Mimosas Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan, kabla ya kushinda kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Tunisia.
  Esperánce sasa itakutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo iliitoa Yanga ya Tanzania kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 0-0 ugenini na nyumbani.
  Mechi za kwanza za Nusu Fainali zitachezwa Aprili 19 na marudiano Aprili 26, Mazembe na Esperance wakianzia nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MAMELODI NA ESPERANCE NA AHLY NA MAZEMBE NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top