• HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2026

    PACOME NA DEPU WAFUNGA YANGA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-0


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
    Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na wachezaji wake wa kigeni, kiungo Muivory Coast, Peodh Pacome Zouzoua dakika ya 52 na mshambuliaji Muangola, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depu’ dakika ya 55. 
    Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 66 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiwazidi pointi mbili watani wao wa jadi, Simba SC baada ya timu hizo zote kucheza mechi 27.
    Kwa upande wao Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 29 kufuatia kucheza mechi 27 pia katika Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PACOME NA DEPU WAFUNGA YANGA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top